Tuesday, June 26, 2018

BAJETI YA TRIONI 32.45 YAPITA KWA KURA 266 ZA NDIYO TANZANIA...82 WAKATAA

  Malunde       Tuesday, June 26, 2018

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni kwa kura 266 kati ya 348 sawa na asilimia 76.Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akitangaza matokeo ya kura leo jioni Juni 26, 2018 amesema jumla ya wabunge waliokuwamo bungeni na kupiga kura walikuwa 348.


“Idadi ya wabunge waliopiga kura 348, wabunge 43 hawakuwepo. Kura za hapana 82 na hakuna kura ambayo haikuamua na kura za ndio ni 266,” amesema Kagaigai


Mara baada ya kauli hiyo, shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM ziliibuka huku Spika wa Bunge Job Ndugai akiwashukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Amesema mara baada ya kuondoka Ijumaa, bila shaka mawaziri wataondoka wakiwa wamesheheni maoni ya wabunge na ushauri ambao kimsingi umetoka kwa wananchi.

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post