MKUU WA JESHI LA POLISI 'IGP' AJIUZULU...RAIS ARIDHIA


Rais wa Gambia, Adama Barrow

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Gambia amelazimika kujiuzulu baada ya watu watatu kuuwawa mapema wiki hii katika eneo la Faraba Banta, kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Banjul, kufuatia polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji.

Wakazi wa mji huo walikusanyika na kuandamana kupinga uchimbaji wa mchanga ambao umekua ukitishia mazingira na mashamba yao ya mchele.

Barua ya kujiuzulu ya Landing Kinteh ilikubaliwa na Rais Adama Barrow jana Alhamisi wiki hii baada ya kukosolewa na upinzani kufuatia vurugu za Faraba Banta. Hata hivyo amedai hakuwaamrisha polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji.

Rais Adama Barrow anatarajia kuzuru mji huo wa Faraba Banta leo ili kukutana na familia za waathirika ambapo pia shughuli za uchimbaji mchanga zimesimamishwa kwa muda.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.