MZEE MAJUTO AREJEA TANZANIA BAADA YA MATIBABU INDIA... " NINGEONDOKA MAPEMA SANA" | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 22, 2018

MZEE MAJUTO AREJEA TANZANIA BAADA YA MATIBABU INDIA... " NINGEONDOKA MAPEMA SANA"

  Malunde       Friday, June 22, 2018

Mchekeshaji maarufu nchini Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto, amefunguka kuwa amepata huduma na matibabu mazuri kutoka kwa madaktari katika Hospitali ya Nchini India na kudai kuwa kama asingefanyiwa matibabu hayo basi angekuwa katika hali mbaya zaidi.

Mzee Majuto amesema hayo leo Juni 22, 2018 akiwa wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuwasili akitokea nchini India, alipokuwa akifanyiwa matibabu ya tezi dume na kuongeza kuwa kuna tofauti ya huduma ya kimatibabu kati ya hapa nchini na alipokuwa India.

“Mimi sijambo nashukuru, Hospitali ni Hospitali isipokuwa wenzetu wapo mbali zaidi, nimefanyiwa mambo mengi sana ambayo kama nisingefanyiwa ningeondoka mapema sana namshukuru Mungu” amesema Majuto.

Mzee Majuto ameongeza kuwa baada ya kumaliza matibabu hayo anataka kutenga muda mwingi kwa ajili ya kupumzika zaidi na kuacha kujihusisha na masuala ya sanaa ya uchekeshaji na kudai kuwa Tanzania bado kuna wachekeshaji wengi ambao wataweza kuendeleza sanaa hiyo.

Muigizaji huyo wa vichekesho kwa sasa amepokelewa na yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mei 4, 2018 Mzee Majuto alisafirishwa kwa gharama za serikali, kwenda nchini India kwa matibabu ya tezi dume baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa kipindi cha muda mrefu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post