HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT AWAMU YA PILI 2018



TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limefanya uteuzi wa awamu ya pili ya wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2018 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.


Vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliopangiwa kuanzia tarehe 14 Juni 2018 hadi tarehe 20 Juni 2018.

JKT linaendelea kusisitiza kuwa ni kosa la kisheria kwa mhitimu yoyote wa elimu ya kidato cha sita aliyeteuliwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria (Compulsory) kukaidi kuhudhuria mafunzo hayo.

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, stadi za kazi stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Orodha kamili ya majina ya vijana walioteuliwa awamu ya kwanza na awamu ya pili, vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo na makambi waliyopangiwa vinapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

BOFYA HAPA CHINI KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA MUJIBU AWAMU YA PILI 2018



MARAMBA-TANGA              MGAMBO-TANGA             MLALE-RUVUMA

MSANGE-TABORA          MTABILA-KIGOMA          NACHINGWEA-LINDI



Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 13 June 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527