AJALI YA HIACE,LORI LA MCHANGA YAUA WATU 14 MKURANGA


Watu 14 wamefarikiki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo Juni 25,2018 saa 10 alfajiri eneo la Dungani wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani baada ya gari la mchanga kugongana na Hiace iliyokuwa inatoka Mkuranga kwenda Dar es salaam.


Mwenyekiti wa kitongoji cha Dungani Mohammed Ngota amesema watu 14 wamefariki dunia huku majeruhi wakiwa wanne wakiwemo watoto wawili.Ajali hiyo imetokea leo Juni 25 saa 10 alfajiri katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Dk Stephen Mwandambo amethibitisha vifo hivyo, amesema maiti za watu 14 zimepokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

"Ni kweli hili tukio limetokea alfajiri, tumepokea miili 14 na majeruhi wanne," amesema Dk Mwandambo.

Kati ya majeruhi hao, amesema mmoja hali yake ni mbaya na walikuwa wanahangaika kuokoa maisha yake.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527