BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA - TEC LAPATA VIONGOZI WAPYA,RAIS NI ASKOFU NYAISONGA

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) leo Jumapili Juni 24, 2018 limemchagua Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga  kuwa rais wa baraza hilo.


Askofu Nyaisonga aliyetangazwa leo Jumapili Juni 24,2018 katika misa ya kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, Beatus Urassa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania mjini humo, amechukua nafasi ya Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa aliyemaliza muda wake.

Ngalalekumtwa amemtangaza Askofu Nyaisonga na kusema atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.


Hivyo Rais Mpya wa TEC ni Mhashamu Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga wa Jimbo la Mpanda, Makamu wa Rais ni Mhashamu Askofu Flavian Kasalla wa Jimbo la Geita na
 Katibu Mkuu ni Fr. Charles Kitima wa Jimbo la Singida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527