Sunday, June 24, 2018

KADINALI PENGO AFUNGUKA KUHUSU MAASKOFU WACHAGA

  Malunde       Sunday, June 24, 2018

Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amewataka maaskofu kuhubiri umoja kwa waumini wao.

Pengo amesisitiza hilo leo Jumapili Juni 24, 2018 katika misa ya kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, Beatus Urassa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania mjini humo na kurushwa moja kwa moja na Redio Tumaini.


“Katika kuliongoza Tanzania ni muhimu sisi maaskofu tusisitize juu ya umoja wa waamini waliokombolewa kwa damu moja ya Kristu. Kwa mazingira ya Tanzania, wewe na mimi na maaskofu wote tusisitize umoja wa Watanzania na Tanzania,” amesema Pengo.

“Tusikubali kuziruhusu damu mbalimbali zinazotufanya kuwa wenye kabila hili au lile zikatawala na kuvunja umoja wa Taifa letu. Tuombeane katika kazi hii. Tutunze umoja wa waumini na wa Taifa letu.”

Amesisitiza, “Wewe umezaliwa mkoani Kilimanjaro ni mchaga unayetoka Rombo. Katika utandawazi wa Tanzania siku hizi ni muhimu kuzingatia yafuatayo, unayo damu ya kichaga ndani ya mwili wako, nakuomba wala usikatae na usijaribu kuificha damu hii.”


“Hakuna sababu wala uhalali kwako wa kujaribu kuficha ukweli huu. Neno moja lazima ulikumbuke ni kuwa wewe na mimi na kundi lote hatujakombolewa kwa damu ya kichaga wala ya kifipa na kinyakyusa, sote tumekombolewa kwa damu ya Kristo.”


Askofu Urassa anachukua nafasi ya Mhashamu Damian Kyaruzi ambaye amestaafu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post