Tuesday, May 8, 2018

WOLPER AMPA MAKAVU SARAH KUMTOSA HARMONIZE

  Malunde       Tuesday, May 8, 2018
Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amemtupia Dongo zito Sarah baada ya habari zake za kumtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond, Mwarabu Fighter.


Siku tatu zilizopita stori iliyotrend kupita zote ni ya mpenzi wa Harmonize Sarah kumtosa mpenzi wake na kumchukua Mwarabu Fighter.


Inasemekana Sarah amekufa ameoza kwa Mwarabu kiasi ya kwamba anamuhudumia ipasavyo yaani kampangishia hadi nyumba yaani zile huduma zozote alizokuwa anapata Harmonize zimehamia kwa Mwarabu.


Kama utakumbuka Kuwa Sarah na Wolper ni maadui wakubwa na kisa kikiwa ni penzi la Harmonize na juzi tu wametoka kumgombania Harmonize.


Baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni Sam Misago Tv walimsaka Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hii kumuhusu Sarah na Wolper ameishia kumtupia dongo zito Sarah:


"Duh iyo ishu mbona ni exclusive kabisa sijaisikia lakini freshi tu mbona yule demu ni Mlezi wa wana labda kachoka kumlea mwana kaamua kumchukua mwana mwingine freshi tu”.


Bifu la Wolper na Sarah lilianza baada ya Sarah kuanza kuchepuka na Harmonize wakati Wolper yupo Kwenye Mahusiano na Harmonize.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post