WEMA SEPETU ALAMBA DILI NONO TATU MZUKA

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameendelea kuwa na mwezi mzuri kwani siku chache baada ya kupata ubalozi wa Kombe la Dunia na Star Times siku ya jana Wema alilamba dili nono na Tatu Mzuka.


Siku ya jana Kampuni ya The Network ambayo inahusika na kuendesha Michezo ya namba ya Tatu mzuka, imetangaza kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na Wema.


Akizungumza Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzima Sebastian Maganga, alisema ushirikiano wao na Wema ni mpango mkakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania ili kuboresha maisha yao.


"Kusudi kubwa la Tatu Mzuka kuingia makubaliano na Wema, ina lengo la kutaka kusambaza fursa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo ili kuboresha maisha yao ya kila siku”.


Lakini pia Wema aliyepata shavu hilo alifunguka na kusema:


"Nina hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha bidhaa hii mashabiki zangu wote na Watanzania kwa ujumla wao ili waweze kujitengenezea fursa nyingi za kuboresha maisha yao kupitia kwangu."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527