Tuesday, May 8, 2018

WAZIRI MWAKYEMBE AZIDI KUMFAGILIA DIAMOND PLATNUMZ

  Malunde       Tuesday, May 8, 2018
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.


“Kwenye tasnia yetu ya sanaa vijana wetu wanaimba nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. 


"Kinacholeta matatizo hapa ni picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. 


"Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. 


"Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao, Diamond yeye haitaji kufanya hivyo”.


Suala hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae kumfungulia.


Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post