Thursday, May 31, 2018

PAPA FRANCIS AWATAHADHARISHA WATAWA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII

  Malunde       Thursday, May 31, 2018
Mtawa akipiga picha na simu ya iPhone

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewaambiwa watawa kutumia mitandao ya kijamii kwa tahadhari.

Waraka huo umetaja mawasiliano ya mitandao ya kijamii, badala ya kusema application husika, lakini Gazeti la kikatoliki application hizo umemaanisha Facebook na twitter.

Onyo la kupoteza muda

Amri ya watawa kaskazini mwa Spain ilisambaa na kuwa kwenye vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii mwezi uliopita kuzungumzia Kesi iliyokuwa na mkanganyiko mjini Pamplona iliyoeleza kundi la wanaume waliokuwa wakishutumiwa kubaka ambapo watu walidai kuwa hukumu haikuwa kali dhidi ya wanaume hao.

Katika ukurasa wao wa Facebook, watawa wa Hondarribia walimtetea mwathirika wa ubakaji kwa kuelezea maamuzi yao huru ya kuishi maisha ya utawa, ya kutokunywa pombe au kutembea nyakati za usiku

''Kwa kuwa ni uamuzi huru, tutatetea kwa namna yeyote tutakayoweza.Haki ya wanawake kuwa huru kutenda kinyume bila kuhukumiwa,kubakwa, kutishiwa au kudhalilishwa kutokana na makosa yake.

Muongozo huu mpya haujatolewa kutokana na kesi hiyo, na hii si mara ya kwanza Kanisa Katoliki kutoa miongozo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watawa.

Katiba ya asili kuhusu maisha ya wanawake watawa, ilichapishwa mwaka 1950 na Papa Pius wa 12, lakini Papa Francis katika toleo la mwaka 2016 ametahadharisha utamaduni wa digitali na namna unavyoathiri jamii.

Amewataka watawa wasifanye mitandao ya kijamii kuwa vitu vya kupotezea muda akisima kuwa Vatican yenyewe huandika sana kwa kutumia mtandao wa Twitter.

Imeweka karibu ujumbe 15,000 kwenye anuani yake mpya ya habari na kuweka zaidi ya mara 1,500 kupitia ukurasa maalumu wa Baba Mtakatifu.

Pia Vatican ina anuani za mtandao wa Facebook,Instagram,You Tube na Google+.
Chanzo-BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post