WANAFUNZI WANAOVAA NUSU UCHI WAPIGWA MARUFUKU KUINGIA MAKTABA

Uongozi wa Chuo kikuu cha Zambia umetoa tangazo la kupiga marufuku kwa wanafunzi wa kike chuoni hapo kuacha kuvaa nguo za nusu utupu hasa wanapoenda maktaba kujisomea.

Tangazo hilo limetolewa jana Mei 07 2018, katika mbao za matangazo ya chuo hicho na kudai kwamba mavazi hayo yanawaathiri wanafunzi wenzao wa kiume ambao wanashindwa kuzingatia kile wanachokifanya wakiwa maktaba.

“Tunatambua baadhi ya wanafunzi wa kike wanavaa nguo za nusu utupu pindi wanapoenda kutumia maktaba, hali ambayo inawagadhabisha wanafunzi wa kiume. Kwahiyo tunashauri wanafunzi wa kike kuvaa nguo za staha pindi unapotumia majengo ya maktaba” imesema sehemu ya tangazo hilo.


Wanafunzi wa chuo hicho wamekua na maoni tofauti kufuatia tangazo hilo ambapo baadhi wameunga mkono agizo la chuo hicho na wengine kupinga kwa kusema kuwa hakuna uhusiano wa nguo fupi na kumuathiri mtu anaejisomea maktaba.

Vyuo vingi vya elimu ya juu Barani Afrika vimekuwa na changamoto ya kudhibiti aina ya mavazi ambayo wanafunzi wanastahili kuvaa wakiwa maeneo ya chuo mfano wa vyuo hivyo ni Chuo kikuu cha Lagos (Nigeria), Zululand (Afrika Kusini) Zambeze (Msumbiji), Al Akhayn (Morocco) , Chuo cha sayansi Misri, na Chuo kikuu cha Ardhi na kile cha biashara (CBE) kutoka Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527