Thursday, May 3, 2018

"SHULE ZA BINAFSI INTEREST YAO NI PESA"-RAIS MAGUFULI

  mtilah       Thursday, May 3, 2018


Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amefunguka juu ya kutofurahishwa na mfumo wa shule binafsi hapa nchini, ambao unaonekana kutowatendea haki wanafunzi wote. 
Rais Magufuli amesema kitendo cha shule binafsi kuwachuja wanafunzi na kuchukua wale wenye uwezo mkubwa zaidi na kuwacha wale wenye uwezo mdogo ni ubaguzi, kitendo ambacho hakiwezi kufanywa na shule za serikali, kwani watoto wote wana haki ya kupata elimu.
Rais Magufuli amesema shule binafsi lengo lake kubwa ni kutengeneza jina na kupata pesa, na sio kufundisha watoto wa kitanzania wawe na elimu sawa.
Shule za private wanachujwa, wale vilaza wanaachwa na kuchukua wale cream ili kusudi wa-secure waonekane wao ndio wanaongoza, serikali inayopenda watu wake haiwezi ikafanya mambo ya kipumbavu hivi. Inachukua watoto wote, ukiangalia tangu mwaka 83 mpaka mwaka huu shule zinazoongoza 10 bora utakuta ni private, kama imebahatika serikali ni moja, tisa ni private, ni kwa sababu ya mlolongo wa wanavyofanya private. Hawako na interest ya kumsomesha kila mtanzania, interest yao ni pesa na kutengeneza jina, hiyo haiwezi kuwa point”, amesema Rais Magufuli.
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni uliibuka mvutano bungeni baina ya Wabunge wakilaumu serikali kuminya shule binafsi, na kuzifanya kutoweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post