Wednesday, May 9, 2018

SHAMSA FORD AMJIA JUU HARMONIZE KUINGILIA NDOA YAKE

  Malunde       Wednesday, May 9, 2018
Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Filamu  Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.


Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.


Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa wa Shamsa Ford kwahiyo baada ya kusikia mumewe katajwa Kwenye orodha hiyo alishindwa kujizuia kwani alikuja juu na kumtaka Harmonize amkome mumewe na asimuingize Kwenye ugomvi wao.


Shamsa alienda kukomenti maneno haya Kwenye posti ya Harmonize:


"Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu pls nisingependa kuona jina la mume wangu Kwenye huo ujinga wenu. Chidi kwenu anaweza akawa mshkaji kwangu mimi ni mume, kulikuwa hakuna haja ya wewe kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tusichukuliane Poa”.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post