MBUNGE AMTAKA WAZIRI ALETE SANGOMA KUPATA MADINI YA MASHETANI

Mbunge wa Newala Vijijini Ajali Akibar amemtaka waziri wa madini Anjela Kairuki kwenda Afrika ya Kusini kutafuta waganga wa kienyeji na kuwaleta nchini, ili kuweza kupata madini kwa wingi.

Mbunge Akibar ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Madini Bungeni, na kusema kwamba amesikia kwamba madini yanatokana na mashetani, hivyo ni vyema Waziri akaenda kumleta mganga aje kuagua.

“Siku moja tuliwahi kusikia kwamba mambo ya madini yanatokana na mashetani, sasa hao mashetani ndio wanaofanya nchi hii isipate madini, kama kweli sisi hatupati madini, basi nikuombe Mheshimiwa Anjela aende South Afrika ukamlete Sangoma aje atuchinjie ili na sisi tuweze kupata madini Tanzania”, amesema Mbunge wa Newala Ajali Akbar.

Mbunge huyo aliendelea kwa kulaumu shirika la Stamico kwa utendaji mbovu, unaosababisha Tanzania kukosa mapato yake kwenye sekta ya madini.
Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527