Thursday, May 24, 2018

MUSUKUMA : WABUNGE 180 NI DARASA LA SABA....HAWASEMI UKWELI WANAFOJI VYETI WAPATE U -WAZIRI

  Malunde       Thursday, May 24, 2018
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma Kasheku ameweka wazi anafahamu zaidi wa Wabunge 180 bungeni darasa la 7 ingawa hawapendi kusema ukweli ndiyo maana wanafoji mpaka vyeti ili kupata nafasi za kuteuliwa U-waziri.

Akichat Live na wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook EATV, Musukuma amesema kwamba viongozi wengi wanaojinasibu kuwa wana elimu kubwa ukikaa nao karibu matendo yao hayafanani na viwango vya elimu wanayoisema.

Aidha Musukuma amefafanua kwamba ifike mahali watu wawe wanawajaji wenzao kwa matendo yao na siyo vyeti kwani watu kuamini kwenye vyeti ndiko kunakopelekea watu kwenda kufoji mpaka vyeti.

"Mimi nafahamu mule bungeni kati ya Wabunge 360 Wabunge 180 ni darasa la saba japokuwa hawataki kueleza ukweli. Wametegesha vyeti ili wapate uwzairi. Unamkuta mtu anavyeti ambavyo huko nyuma hakuwa navyo. ukifatilia historia kabla ya kuingia bungeni alikuwa Jobless wengine ma DJ na elimu wanazizisema sijui Cambridge hawana".

Pamoja na hayo Musukuma amesema pamoja na kuwa alisha declare yeye ni darasa la saba ipo siku ataweka wazi kiwango cha elimu yake na kwamba licha ya kuwa ana elimu hiyo yeye ni mtu ambaye anapenda kusoma na ana uelewa wa kupambanua mambo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post