Thursday, May 24, 2018

JAJI AAMURU KIJANA ALIYENG'ANG'ANIA NYUMBANI KWA WAZAZI AONDOKE

  Malunde       Thursday, May 24, 2018
Michael Rotondo ameamriwa na Mahakama kuondoka nyumbani kwa wazazi wake

Wazazi wawili mjini New York wameshinda kesi waliyokuwa wakipambana kumuondoa kijana wao mwenye umri wa miaka 30 baada ya kukaidi kuondoka.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya juu ya jimboni humo, Jaji aliamuru kijana huyo aondoke nyumbani kwa wazazi wake.

Jaji Donald Greenwood alimwambia kijana huyo kuendelea kubaki nyumbani kwa miezi sita zaidi kama alivyoomba ''haikubaliki''

kijana Michael Rotondo ambaye alijiwakilisha mwenyewe mahakamani, amesema ''Sijui kwa nini hwawezi kusubiri kidogo kabla ya mimi kuondoka,Bwana Rotondo alieleza huku wazazi wakiwa wamekaa karibu na mwanasheria wao wakimtazama.

Alisema kuwa miezi sita ndio muda uli sawa kwa mtu ambaye alikuwa akiwategemea watu .Wazazi wa Michael Christina na Mark Rotondo

Jaji akiwa anatabasamu alimtaka kijana huyo azungumze na wazazi wake,na kuamua kwa hiyari kuondoka nyumbani, lakini Rotondo alikataa.

''Nataka uondoke hapo nyumbani'' Jaji Greenwood aliamuru, kwa mujibu wa kituo cha habari cha ABC

Walipokuwa wakifungua mashtaka juma lililopita,Christina and Mark Rotondo walionyesha nakala ya nyaraka walizokuwa wakimuamuru kuondoka nyumbani tangu tarehe 2 mwezi Februari mwaka 2018.

Sehemu ya nakala zikiwa zimeandikwa ''Kuna kazi zinapatikana hata kwa wale wenye historia mbaya ya kufanya kazi kama wewe'' ''Nenda katafute kazi-unapaswa kufanya kazi!''Makazi ya familia ya Rotondo, NewYork

Pia wazazi hao walimpatia dola za Marekani 1,100 ili aondoke nyumbani, kwa mujibu wa barua walimtaka auze baadhi ya vitu vyake ikiwemo gari yake mbovu aina ya Volkswagen Passat.

''Nilitumia na wala sijutii, alieleza waandishi wa habari kuwa alizitumia pesa hizo

Mahakamani Rotondo alikiri kuwa hakuwahi kuchangia gharama zozote nyumbani.

Baada ya kusikilizwa kwa kesi siku ya Jumanne , Bwana Michael Rotondo aliwaambia waandishi wa habari kuwa atakata rufaa, na amepanga kuondoka nyunbani miezi mitatu ijayo.

Michael Rotondo amesema uhusiano na wazazi wake haujawa mzuri, kiasi cha kutozungumza kabisa ndani ya nyumba.

amesema wazazi wake walimwambia kuwa anaweza kuishi nao miaka minane iliyopita alipopoteza kazi.

Alisema kwa sasa ana kazi , alipoulizwa kuhusu kazi anayofanya alikataa kutoa maelezo zaidi.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post