MBUNGE WA SHINYANGA MJINI ACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).


Taarifa hiyo imetolewa leo asubuhi Mei 11, 2018 bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa jana kwa kishindo.

“Umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM).

“Nampongeza sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana Rais John Magufuli.”
Mheshimiwa Stephen Masele akiwa na Watanzania waishio Afrika Kusini




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527