MBUNGE WA CCM AIPONDA SERIKALI

Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya (CCM), Livingstone Lusinde amefunguka na kuiponda serikali kuwa inashindwa kusimamia mambo yake vizuri jambo ambalo linapelekea matumizi ya fedha kuwa makubwa huku miradi ikikwama.


Lusinde amesema hayo leo bungeni wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa serikali imekuwa ikishindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha jambo ambalo linazidi kuturudisha nyuma kimaendeleo.


"Waziri akinisikiliza vizuri anaweza kuona namna ambavyo serikali wakati mwingine inashindwa kusimamia matumizi mazuri ya fedha kwani ikisimamia vizuri fedha thamani ya fedha itaonekana na tutapata maji mengi na kwa uhakika 


"Kwa mfano watu wa WFP wametupa milioni mia saba tisini na tisa kwenye jimbo la Mtera, kwa fedha hizo hizo tumepata matenki makubwa ya lita laki nane matatu, tumepata visima kumi na nane, tumepata mashamba heka mia tatu kwa ajili ya umwagiliaji, tumepata visima kumi na mbili vilivyofungwa solar Power kwa ajili ya wananchi kupata maji hebu angalia matumizi haya ya fedha hizi yameleta vitu vikubwa ambavyo wananchi wananufaika lakini ukija kwenye serikali hakuna kitu"


"Kwenye serikali inatolewa bilioni moja pale Kwayungu kwa ajili ya kujenga bwawa la umwagiliaji mpaka sasa bwawa halijakamilika, hakuna miundombinu na bilioni imeliwa 


"Kwa hiyo unaweza kuona matumizi mabaya kwenye miradi ya maji kwa upande wa serikali ndiyo yanatuletea matatizo makubwa... hawa wametoa milioni 800 wametengeneza mambo ambayo ni maajabu kabisa.


" Mhe Waziri na Katibu Mkuu piteni muone namna ambavyo pesa ikisimamiwa hata ikiwa kidogo inaweza kufanya vitu vikubwa watu saizi wanapata maji ya kunywa, wanamwagilia na maisha yao yapo safi" alisisitiza Lusinde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527