Mbunge
wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM), amesema kuna haja ya serikali
kusitisha ulaji wa samaki nchini kama uvuvi wa samaki hautakiwi.
Amesema
pamoja na kwamba serikali inapiga vita kupitia operesheni sangara
katika Ziwa Victoria, operesheni hiyo haiwezi kukubaliwa kwa sababu
inaumiza wavuvi.
Kishimba ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha wa 2018/19.
“Mji
wa Mwanza umejengwa kupitia pamba na madini, na hao samaki wanaopigwa
marufuku kuvuliwa nao wamechangia kwa sehemu kubwa ukuaji wa mji huo
naiomba serikali iwagawie wavuvi vifaranga wa samaki ili zao la samaki
liweze kuinufaisha serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema.