Makubwa haya : MWANASAYANSI AANZA SAFARI KWENDA KUJIUA..AJUTIA KUISHI

David Goodall anasema anataka kufa kwa heshima

Mwanasayansi mwenye umri wa miaka 104 David Goodall ameaga nyumbani Australia kuanza safari ya kimataifa kwenda kujitoa uhai.

Sio kwamba mwanaekoljia huyo anaugua mahututi, La, anatamanai kuharakisha kifo chake. Sababu kuu ya uamuzi wake anasema ni kupungua kwa uhuru wake.

"Najuta kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia.

"Sina raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu anazuiwa kufa."

Ni jimbo moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua mahututi.

Dkt Goodall anasema atasafiri kwenda katika kliniki moja nchini Uswisi kujitoa uhai kwa hiari. hatahivyo anasema anachukizwana kwamba anaondoka nyumbani ili aweze kufanya hivyo.Carol O'Neill anaandamana na Dkt Goodall katika safari yake Ulaya kwenda kujitoa uhai

Je ni mataifa gani mengine yanaruhusu kujitoa uhai?
Uswizi, ni nchi pekee iliyo na vituo vinavyotoa huduma hiyo kwa raia wa mataifa mengine.
Uholanzi, Ubelgiji na Luxembourg zinaruhusu, hata kwa watoto lakini katika hali maalum.
Colombia inaruhusu kujitoa uhai kwa hiari wakati mgonjwa akiwa hatibiki.
Majimbo sita ya Marekani - Oregon, Washington, Vermont, Montana, California na Colorado - zinaruhusu kwa wagonjwa mahututi wasio tibika.
Canada ililifuata jimbo la Quebec kuruhusu hilo mnamo 2016.Jamaa zake Goodall watajumuika naye huko Uswizi
Mjadala unazusha mgawanyiko Afrika

Katika nchi nyingi tu Afrika, njia zote za kujitoa uhai zinatizamwa kama mauaji.

Wataalamu barani Afrika wamepinga wito wa watu kutaka kujitoa uhai kwa hiari.

Mjadala mkubwa umezuka kuhusu kinachotajwa kuwa 'kuuawa kwa huruma' hususan kwa wagonjwa walio mahututi na wasioweza kutibika.

Lakini mkutano wa muungano wa wataalamu wa afya duniani katika mkutano mapema mwaka huu mjini Abuja NIgeria waliamua kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume na kiapo cha matabibu na inakwenda kinyume na imani na maadili ya jamii za Kiafrika.

Badala yake viongozi katika muungano hao wameyaka kuboreshwa kwa huduma za kuwashughulukia wagonjwa mahututi wasioweza kutibika.

Masuala yaliozingaiwa katika kuptisha uamuzi huo ni sheria, dini, jamii na tamaduni, saikolojia na upana wa maadili kuhusu suala hilo.

Wataalamu wa mataifa kutoka Afrika kusini, Kenya, Botswana, Zambia na Cote D'ivore walipinga hoja hiyo ya kujitoa uhai kwa hiari wakisisitiza inakwenda kinyume na maadili ya utoaji matibabu.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527