KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AGOMA

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amegoma kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa madai kuwa thamani ya fedha za ujenzi zilizotumika haziendani na nyumba hizo.

Tukio hilo limetokea leo Mei 8,2018  baada ya kiongozi huyo kutembelea mradi huo wakati mwenge wa Uhuru ukikimbizwa wilayani Kalambo huko mkoani Rukwa.

Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo unaotajwa kuwa na thamani ya Sh511milioni,akibainisha kuwa kuna matumizi mabaya ya fedha za umma. 

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi huo uliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo, Simon Kagani amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 2016 na kukamilika Aprili 2017 na kugharimu kiasi hicho cha fedha, ambapo Serikali Kuu imechangia Sh496milioni, halmashauri Sh15milioni.

Akitaja sababu za kutozindua mradi huo ni kwa kuwa amebaini thamani ya fedha haifanani na nyumba zilizojengwa na kwamba milioni 500 imetumika kujenga nyumba tani ambazo hazina thamani hiyo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.