KIJANA ALIYEUA MCHUMBA WAKE KWA KISU ALAZIMISHWA KUOA MAITI

Kuna hii habari kuhusu Familia ya marehemu Confidence Nwanma ya nchini Nigeria ambaye inadaiwa alichomwa kisu na kuuawa na mpenzi wake katika ugomvi wao, familia ya Marehemu sasa imemtaka jamaa huyo kuandaa harusi ya kitamaduni na maiti ya mtoto wao kabla ya mazishi. 

Saliu Ladayo alijisalimisha polisi na kudaiwa kukiri kumuua Confidence katika nyumba yao. Akizungumza na waandishi habari, baba mzazi wa Marehemu, Jude Nwanmaamesema kuwa Ladayo lazima achukue mwili wa marehemu na kumpeleka katika kijiji chao ili amuoe kabla kuzikwa. 

‘’ Kwetu ni lazima mwanaume aoe maiti ya mwanetu kabla kuzikwa. Lazima tufuate kanuni hiyo kwa kumpelekea maiti katika kijiji kutakapofanyika harusi. Ni lazima alipie mahari maradufu maana alimleta binti yetu akiwa maiti’’ Baba wa marehemu 

Aidha Baba wa marehemu alitoa onyo kali kwa kijana huyo iwapo harusi hiyo haitafanyika. 

‘’ Lazima atafuata kanuni zote kabla familia yetu kumuacha. La sivyo kila mmoja katika familia ya kijana huyo atafariki kabla kufika umri wa binti yetu aliyefariki. Watafariki sawa na binti yetu.’’ Aliongezea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527