AFARIKI KWA KUTUMBUKIA MTONI AKIJIPIGA SELFIE


Kijana mmoja ambaye hakujulikana jina mara moja nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kutumbukia mtoni wakati akijaribu kujipiga picha kwa simu maarufu kama 'Selfie'.

Tukio hili limetokea eneo la Nembe katika mji wa Bayelsa, ambapo kijana huyo alikua anajaribu kupiga picha ya mwisho ya kumbukumbu katika chuo cha mafunzo ya usalama NYSC.

Wakisimulia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamesema kwamba mtu huyo aliteleza kwa bahati mbaya wakati walipokuwa amesimama eneo la “Jetty” katika mto huo na kutumbukia mtoni.

Mwili wa kijana huyo ulipatikana dakika 30 baada ya kuzama na hakuna taarifa za kumtambulisha mtu huyo.


Mamlaka za mji huo zimeshindwa kumtambua mtu huyo na hakuna ndugu wala jamaa ambaye amekwisha jitokeza hata baada ya picha za mtu huyo kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527