Saturday, May 12, 2018

ALIYETAKA KURITHI PENZI LA DIAMOND KWA ZARI AAIBIKA NA GARI LAKE JIPYA AKITAKA KUHONGA

  Malunde       Saturday, May 12, 2018
Zari The Boss Lady amesema hamfahamu Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya aliyetangaza kumnunulia mrembo huyo gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017.

Hapo jana Ringtone Apoko aliweka wazi kuwa amenunua gari hilo baada ya kusikia Zari atawasili nchini humo kwa ajili ya event yake, pia kipindi cha nyuma msanii huyo alipopata taarifa za Zari kuachana na Diamond alijitokeza na kueleza ana nia ya kumuoa.

 Zari akiwa nchini Kenya amehojiwa na kituo cha Radio, Kiss FM na kueleza kuwa hamfahamu msanii huyo.

“I don’t know ringtone and I have never met him. This is actually news to me. I have over 3.9 million followers on instagram and I wouldn’t know who follows me,” Zari  said.

“Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi,” amesema Zari.

Zari yupo nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ itakayofanyika weekend hii Uhuru Gardens.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post