ALIKIBA ALIAMSHA DUDE...AACHIA NGOMA KALI INAITWA "MVUMO WA RADI..ITAZAME HAPA


Msanii wa BongoFleva Alikiba maarufu kama King Kiba ameweza kutimiza moja ya ahadi yake aliyowapa mashabiki kwa kutoa wimbo mpya hii leo uliopewa jina la 'Mvumo wa Radi' kama alivyoahidi hapo awali.


Alikiba alitoa ahadi hiyo mnamo Mei 2, 2018 kupitia mtandao wake wa kijamii instagram mara baada ya Ommy Dimpoz kuachia ngoma yake ya 'Yanje' aliyomshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria licha ya video hiyo kutofikisha watazamaji milioni 3 kama alivyotaka iwe.

Wimbo huu, Alikiba ndio wa kwanza kuachia tangu alipoingia katika ulimwengu mpya wa ndoa siku za hivi karibuni huku mashabiki zake wakimpongeza msanii huyo kwa kuweza kubadilika badilika kila anapoamua kurudi tena katika muziki.

Kama hujapata bahati ya kutazama video mpya ya Alikiba tazama hapa chini.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.