Friday, May 11, 2018

ALIKIBA KUOA MKE WA PILI?? MKEWE AFUNGUKA

  Malunde       Friday, May 11, 2018
Amina Khalef mke wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amesema suala la mumewe kuoa mke wa pili anamuachia Mungu.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 11, 2018 katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa Redio Clouds, Amina ambaye alionekana kuwa mzito kutoa majibu mpaka alipobanwa na watangazaji waliokuwa wakimhoji, amesema suala hilo anamuachia Mungu.


Kwa upande wake Ali Kiba alipotakiwa kuzungumzia jambo hilo amesema ataoa kama mkewe ataridhia kufanya hivyo na kuongeza kuwa kwa sasa angependa kuwa na Amina pekee.

Leo asubuhi wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, Ali Kiba amesema wanawake wanaopenda awaoe wasubiri kwa kuwa ana nafasi tatu za kuoa, kama ambavyo dini inamruhusu.


Alipochomekewa swali kama miongoni mwa wanawake hao ni mrembo, Jokate Mwegelo ambaye inatajwa kuwa aliwahi kuwa na uhusiano naye, Ali Kiba alikwepa swali hilo na kubainisha kuwa kwa sasa ni mume wa mtu.

Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Aprili 19, 2018 mjini Mombasa, na kisha kufanya sherehe nyingine kubwa nchini iliyohudhuriwa na mstaa kibao.


Amina pia alieleza jinsi alivyokutana na msanii huyo na kubainisha kuwa mara ya kwanza ilikuwa kwenye ndege, kwamba wakati huo hakuwa akimjua.

Amesema mara ya pili binamu yake alimkutanisha na Ali Kiba na hapo ndipo walipoanza uhusiano.


Amesema siku Ali Kiba alipomtamkia kuwa anataka kumuoa, alimtaka aende kwa wazazi wake akajitambulishe, jambo ambalo msanii huyo aliliridhia.


“Nyimbo yake inayonivutia ni Aje aliyoitoa mwaka mmoja uliopita,” amesema Amina.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post