Friday, May 11, 2018

EBITOKE : NIKIFUMANIA NA - DEAL NA MWANAMKE SIYO MWANAUME

  Malunde       Friday, May 11, 2018
Mchekeshaji wa kike bongo Ebitoke amewapa somo wanawake nini cha kufanya pale wanapofumania wapenzi au waume zao ili kuendelea kubaki nao na sio kuishia kuachwa.

Akiwa KIKAANGONI East Africa Television, Ebitoke amewaambia wanawake kwamba wajue wanaume ni watu wanaotaka kwenda nao kwa upole na sio kuwakaripia, hivyo linapotokea suala kama hilo la msingi ni kumuuliza mwenzi wako kwa upole na ku-deal na mwanamke ambaye amekuchukulia mali yako.

“Sasa ukigombana na mwanaume akikuacha je, mi napambana na mwanamke amuache yeye, siwezi kumuacha bwana wangu, nitamuuliza kwa utaratibu tu, unajua mwanaume ili awe mpole kwako lazima uende nae kipole kipole, sasa unatakiwa u-deal na mwanamke bila kumuhusisha, hata kama yeye ndio kasababisha”, amesema Ebitoke

Ebitoke amesisitiza kwamba iwapo yeye atamfumania mpenzi wake na mwanamke mwengine, hatohangaika na mwanaume wake, isipokuwa atamshikisha adabu yule mwanamke ili amuache mwanaume wake.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post