Friday, May 18, 2018

AFANDE WA SHAMBULIO LA AIBU AHAMISHWA

  mtilah       Friday, May 18, 2018
Jana May 17, 2018 Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya uteuzi na mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa polisi wa mikoa katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa jeshi la polisi nchini Barnabas Mwakalukwa imesema IGP Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi Maulid Mabakila aliyekuwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha kuzuia uhalifu Makao makuu ya Polisi DSM kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar.

IGP Sirro pia amefanya mabadiliko kwa Makamanda wa  Mikoa ambapo Naibu DCI Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ng’anzi ameteuliwa kuwa RPC wa Arusha huku RPC Arusha Charles Mkumbo akihamishiwa Makao Makuu.

Pia aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali amehamishiwa Kaskazini Pemba na nafsi yake ikichukuliwa na Kamishna na msaidizi Thobias Sedoyeka.Kamanda Hassan Nassir Ali alizishika headlines za vyombo vya habari Tanzania Baada ya kusambaa kwa video aliyokuwa  anazungumzia suala la kuwa kamata na kuwafikisha mahakamani wanaume wanao jikoolesha au hata kuwasumbua wanawake wenye maumbile makubwa haswa sehemu za nyuma
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post