Saturday, April 28, 2018

WAZIRI SHONZA ASEMA 'MWANAUME MASHINE ' HAUJAFUNGIWA

  Malunde       Saturday, April 28, 2018
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema wimbo wa Mwanaume Mashine haujafungiwa.

Ametoa kauli hiyo jana jioni Aprili 27, 2018 baada ya jana mchana Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuhoji sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Shonza ametoa kauli hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 baada ya Zungu kutaka kupewa jibu kuhusu ‘Mwanaume Mashine’ kutokana na maelezo ya Shonza na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wanajibu hoja za wabunge kuhusu bajeti hiyo kutoeleza sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.

Mchana Zungu alihoji kufungiwa kwa wimbo huo wakati unamtaja mchezaji mahiri wa Simba.

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post