WABUNGE WA CCM,MTULIA NA MOLLEL WAAPISHWA BUNGENI

Naibu Spika, Tulia Ackson, leo amewaapisha wabunge wawili, Dk Godwin Mollel wa Siha na Maulid Mtulia wa Kinondoni, leo Aprili 3,2018.


Wabunge hao wameapishwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni, baada ya wabunge wa maeneo hayo kuhamia CCM.


Mtulia, alikuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa kupitia CCM.


Kadhalika Mollel, alikuwa mbunge wa Siha, (Chadema) kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.


Hata hivyo kiapo hicho hakikushuhudiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo katika kikao cha leo.


Hili ni bunge la kumi na moja na mkutano wa kumi na moja.


Na Habel Chidawali,Mwananchi














Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527