UVCCM KIGOMA,BODABODA WAENZI MUUNGANO KWA MCHEZO...DC JENERALI GAGUTI AFUNGUKA


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26 kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi na bodaboda bila kujali itikadi za vyama vyao.


Pongezi hizo alizitoa jana mara baada ya mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma Ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi  ambapo vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM waliibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya timu ya Vijana wa Bodaboda na kuwapatia kila timu mbuzi mmoja na mchele kilo 20 kwa ajili ya kudumisha na kuuenzi Muungano.

Brigedia Gaguti alisema vijana hao wameonyeshamfano mzuri wa kuigwa na wameienzi falsafa ya Muungano kwa kitendo walichokifanya na kuwataka vijana hao kuendelea kudumisha umoja na mshikamano hata katika maendeleo ili kuhakikisha mkoa wa Kigoma unasonga mbele na kwa kufanya kazi na kujituma pamoja na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

"Nitoe pongezi kwa vijana wa Kigoma kwa viongozi wa UVCCM na bodaboda kwa hili mlilolifanya la kudumisha Muungano na kuuenzi na kuudumisha , lakini kubwa zaidi mmetoa funzo kwa mchezo huu mlioufanya hili ni funzo hata kwa vijana wengine na watanzania wote mnatakiwa kuishi kwa ushirikiano sio kwa michezo tu hata katika mambo mengine ya maendeleo ilituweze kuendeleza umoja, mshikamano na uzalendo kama Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu", alisema mkuu huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM mkoa wa Kigoma Silvia Sigura alisema wao kama viongozi wa vijana walibuni mchezo huo katika sikuku ya Muungano lengo likiwa ni kuwaunganisha vijana wa mkoa wa Kigoma kuwa wamoja na kuendeleza ushirikiano katika kuuinua mkoa wa Kigoma.

Alisema michezo ni afya na ni kitu kinachoweza kuwaunganisha vijana kwa umoja na kuendelea kushirikiana katika mambo mbali mbali na kuwaomba vijana kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri ili kudumisha amani na mshikamano wa taifa la Watanzania bila kuangalia vyama vyao na kuendeleza umoja na mshikamano katika kazi na mambo mbali mbali ya kijamii.

Nao baadhi ya vijana wa boda boda walioshiriki katika mchezo huo January Exavery alisema wanaushukuru sana uongozi wa UVCCM mkoa wa Kigoma kwa kuandaa mchezo huo wa kirafiki na kuomba ushirikiano huo waliouanzisha uendelee na kuwaasa vijana wengine waachane na ushabiki wa vyama vya siasa kwa kufanya mambo yasiyo na msingi na wafanye kazi.

Alisema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata hiduma bora na maendeleo na kuwaasa vijana kiwa wakati huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kushirikiana na sio wakati wa kukaa vijiweni na kuzungumzia siasa zisizo na maendeleo na wafanye kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza wakati wa mchezo huo - Picha zote na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza
Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akifuatiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM mkoa wa Kigoma Silvia Sigura



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527