Tanzia : ABBAS KANDORO AFARIKI DUNIA

 Mkuu wa mkoa mstaafu Mzee Abbas Kandoro amefariki dunia usiku huu wa Ijumaa Aprili 27,2018 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikolazwa kwa matibabu.

Kabla ya kifo chake aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya na mikoa mingine.

Siku mbili zilizopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimtembelea na kumpa pole Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambapo awali alikuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kabla ya kuhamishiwa Muhimbili Dar es salaam ambapo umauti ndipo ulipomkuta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527