Taharuki Shinyanga : ALIYEVAA KIASKOFU NA KUSHIKILIA BIBLIA ,MAJEMBE AZUIA MAGARI BARABARANI,ADAI KATUMWA NA MUNGU..TAZAMA PICHA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 7, 2018

Taharuki Shinyanga : ALIYEVAA KIASKOFU NA KUSHIKILIA BIBLIA ,MAJEMBE AZUIA MAGARI BARABARANI,ADAI KATUMWA NA MUNGU..TAZAMA PICHA

  Malunde       Saturday, April 7, 2018
Taharuki ya aina yake imetokea katika eneo la Sisi kwa Sisi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza mjini Shinyanga baada ya mwanaume ambaye hajajulikana jina wala makazi yake aliyevaa nguo nyekundu zinazodaiwa kuwa za kiaskofu akiwa amebeba,biblia na silaha za jadi ikiwemo msumeno na majembe yaliyochomelewa kisha kusimamisha magari yaliyokuwa yanapita barabarani.

Tukio hilo lililodumu kwa takribani dakika 45 limetokea leo Jumamosi Aprili 7,2018 saa tano asubuhi.

Mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 40 alikuwa amevaa nguo nyekundu,kofia nyekundu yenye msalaba,biblia,mito,midoli,msumeno,baiskeli na majembe yenye mipini ya nondo.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa jamaa huyo alifika katika eneo la Ushirika karibu na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kisha kusimama kwenye eneo la kuvukia ‘Zebra’ akaanza kusimamisha magari.

“Alifika hapa akiwa amevaa joho jekundu kama la kiaskofu pamoja na kofia nyekundu yenye msalaba huku akiwa ameshikilia biblia,baiskeli,msumeno na majembe,akatandaza barabarani vitu alivyokuwa navyo akawa anasimamisha magari huku akisema yeye ni Malkia wa Nguvu ametumwa na Mungu kuja Kukomboa nchi ya Tanzania,wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.

Aidha wamesema wakati akisimamisha magari alisikika akisema bado usiku ,hapajakucha wasiendelee na safari na kwamba yeye ametumwa kuja kukomboa nchi.

“Alisimamisha kila gari pande zote mbili,akasababisha foleni ndefu,dereva wa basi la Mgamba lililokuwa linatoka Mwanza alipogoma kusimama ndipo jamaa akapasua kioo cha mbele akitumia majembe yake ambayo yamechomelewa nondo”,waliongeza mashuhuda.

Kufuatia taharuki hiyo jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata mwanaume huyo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote akisema wampeleke tu kwenye vyombo vya sheria kwani yeye hana kosa bali amekuja kukomboa nchi.

Hata hivyo inaelezwa kuwa jana jamaa huyo ambaye hajulikani ametokea wapi alionekana eneo la Ushirika akiwa amevaa kanzu nyeupe na kofia 'kibaraghashia' na hata juzi alifika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zilizopo hapo Ushirika.

Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde amefika katika eneo la tukio ametusogezea picha za matukio
Mwanaume aliyevaa nguo nyekundu baada ya kuvua joho jekundu akiwa amesimama katika eneo la kuvukia Zebra eneo la Ushirika barabara ya Shinyanga - Mwanza baada ya kuvua joho lake jekundu na kubakiza tisheti na kaptura nyekundu . Pichani ni vifaa alivyokuwa navyo ikiwemo baiskeli,mfuko mwekundu,biblia,midoli,biblia na nguo nyekundu -Picha na Malunde1 blog
Jamaa akichezea mdoli barabarani
Mwanaume huyo akiwa ameshikilia msumeno na jembe akizuia magari yasipite
Jamaa akisimamisha magari
Jamaa akisimamisha mabasi
Jamaa akisimamisha basi
Askari polisi wakimwondoa barabarani jamaa huyo akiwa amevaa nguo nyekundu na kofia yenye msalaba
Askari polisi akiokota vifaa vya jamaa huyo ambavyo ni biblia,mto,nguo na mdoli
Askari polisi akiwa ameshikilia majembe ya jamaa huyo
Askari polisi akiruhusu magari yaendelee na safari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuondolewa barabarani.Nguo nyekundu hapo chini ni joho lake la kiaskofu alilolivua baada ya kuanza kusimamisha magari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi 
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Askari polisi wakimpeleka jamaa huyo kwenye gari la polisi
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Jamaa akipanda kwenye gari la polisi
Askari polisi akiwa ameshikilia msumeno na majembe mawili ya mwanaume huyo
Jamaa akiwa kwenye gari la polisi
Wananchi wakishuhudia tukio hilo
Mwanaume huyo akiondoka na polisi
Picha kwa hisani ya Malunde1 blog


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post