SPIKA NDUGAI :TUNDU LISSU ALIPELEKWA KUTIBIWA NAIROBI BILA KUFUATA UTARATIBU...WAJERUMANI WANAMSAIDIA

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ili mbunge aweze kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za Bunge anapaswa kuwa na vibali vitatu; kibali cha Bunge, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Rais John Magufuli.


Ametoa kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge kushindwa kutoa gharama za matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki, Tundu Lissu.

"Kuna siku nitataja orodha ya wabunge wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe na vibali hivi. Rais alishasema wazi kuwa anazuia safari za nje zisizokuwa na lazima. Lissu alipelekwa Nairobi katika matibabu kwa utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo nimeshalisema sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza:

“Nashukuru Lissu anaendelea na matibabu na ninajua kuna Wajerumani wanamsaidia."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527