RAIS MSTAAFU ATANGAZA NDOA NA BINTI WA MIAKA 24

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameushangaza umma baada ya kuwepo na taarifa za kutarajia kuoa mke wa tano, binti mdogo mwenye umri wa miaka 24.


Taarifa hizo zimethibitishwa na binti huyo ambaye ni mke mtarajiwa wa Zuma anayejulikana kwa jina la Nonkanyinso Conco, kupitia chombo cha habari cha Times live cha nchini Afrika Kusini.


“Ndio tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa kabla sijafanya interview (mahojiano) yoyote”, amesikika binti huyo akiuambia mtandao wa Times Live.


Habari zaidi zinasema kuwa binti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na Jacob Zuma ambaye amezaliwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Jacob Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa.


Jacob Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara sita, na hii itakuwa ni mara ya saba kufunga ndoa,


Tukio hilo limeonekana kuwakwaza wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma, kwani wana tofauti ya miaka 52.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527