Thursday, April 26, 2018

RAIS MAGUFULI AITANGAZA DODOMA KUWA JIJI JIPYA

  Malunde       Thursday, April 26, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 26, 2018 ameupandisha hadhi mji wa Dodoma na kuwa jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wananchi walioweza kujitokeza katika viwanja vya Jamhuri vilivyopo Dodoma ambapo ndipo zilipofanyikia sherehe za miaka 54 ya Muungano kitaifa.

"Azma ya serikali kuhamia Dodoma ipo pale pale hakuna kurudi nyuma na tayari zaidi ya watumishi 3800 wameshahamia na mimi kama nilivyo ahidi mwaka huu nahamia Dodoma. Dodoma ndio makao makuu kwa hiyo kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa watanzania Dodoma ni Jiji", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "kwa hiyo maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hili jipya na hili litakuwa Jiji la pekee yake kwasababu lipo kati ya Tanzania".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa wako safi bila ya kujali vyama vyao.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post