FC BARCELONA YATWAA TAJI

Klabu ya FC Barcelona ya Hispania usiku wa April 21 2018 ilicheza mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey dhidi ya Sevilla katika uwanja wa Wanda Metropolitano wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 68000.

FC Barcelona wakicheza mchezo wao wa fainali ya Copa del Rey kwa mara ya nne mfululizo wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa kupata ushindi wa magoli 5-0, magoli ya FC Barcelona yakifungwa na Luis Suarez dakika ya 14 na 40, Lionel Messi dakika ya 31, Andre Iniesta dakika ya 52 na Philippe Coutinho kwa mkwaju wa penati dakika ya 28.

Ushindi huo wa 5-0 wa FC Barcelona unaifanya timu hiyo kutwaa taji la nne mfululizo la Copa del Rey, huku nahodha wao Andre Iniesta leo akitwaa taji lake la 31 kwa mashindano yote akiwa na club ya FC Barcelona.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.