BUNGE LA BAJETI LAANZA DODOMA

Mkutano wa 11 wa Bunge, ambao ni mahsusi kwa ajili ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2018/2019, unaanza leo mjini Dodoma bila Spika wa Bunge Job Ndugai, ambaye yuko nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Ndugai yuko nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka huu akipatiwa matibabu na hakuwapo hata wakati wa Mkutano wa 10 ulioongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson na Wenyeviti wa Bunge.

Hata hivyo, Bunge lilithibitisha jana (Aprili 02, 2018) kuwa Ndugai hata kuwapo mwanzoni mwa mkutano huo na atarajiwa kurejea nchini wakati wowote kuanzia sasa.

Mbali na Ndugai, mkutano huo unaanza bila kuwapo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ambaye yuko rumande pamoja na wabunge wengine wa chama hicho kutokana na kukabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo ya kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

Wabunge wengine ni Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Mnyika (Kibamba), Esther Matiko (Tarime Mjini) na viongozi wengine wa Chadema ambao ni Katibu Mkuu Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.

Pia Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, alipokuwa akitoka Afrika Kusini kwa matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527