AJALI YA POLISI NA WANAJESHI YAUA MOROGORO

Gari la askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa wametoka katika sherehe za miaka 54 ya Muungano Dodoma, limepata ajali baada ya kuigonga gari aina ya Noah na kusababisha vifo vya watu wawili leo Aprili 27,2018.


Waliofariki, ni waliokuwa kwenye Noah, akiwamo mtoto miezi tisa, Amina Hassan na dereva wa Noah, Zindao Cornell, askari wa JWTZ.

 Kamanda wa Polisi, mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema gari lililokuwa limebeba askari wa JWTZ, lilipata hitilafu katika tairi na kuigonga Noah.


“Ni tatizo la kiufundi, kwa sababu gari lililobeba wanajeshi lilipata hitilafu ya kukakamaa kwa tairi la mbele, gari hilo likamvuta dereva upande wa kulia na likagonga Noah,” amesema.


Amesema askari sita wa JWTZ, walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.


Kadhalika ameongeza kuwa mama mwenye mtoto wa miezi tisa, amelazwa katika hospitali hiyo.

Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527