WAFUASI WA CHADEMA WALIOKAMATWA MSIBANI WAFIKISHWA MAHAKAMANI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 14, 2018

WAFUASI WA CHADEMA WALIOKAMATWA MSIBANI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

  Malunde       Wednesday, March 14, 2018

Wafuasi zaidi ya 10 wa Chadema waliokamatwa wakiwa nyumbani kwa mwanachama mwenzao kuhani msiba wanatarajiwa kupandishwa kizimbani muda mfupi ujao.


Watu hao, leo Machi 14, 2018 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza na kuwekwa katika mahabusu mahakamani hapo kusubiri kukamilika kwa taratibu za kimahakama ili wasomewe mashtaka dhidi yao.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi watu hao walikamatwa eneo la Mabatini Machi 13, 20018 baada ya kutokea kutoelewana kati yao na askari polisi.


Amesema askari hao walikuwa wakifuatilia nyendo za wafuasi hao tangu walipokuwa wakikusanyika kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Mwanza kwenda nyumbani kwa wanachama mwenzao kwa kile kinachodaiwa ni kuhani msiba.


Katika tukio hilo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu zaidi ya 500 waliokuwa kwenye eneo hilo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post