MBUNGE AKAMATWA KWA KUPANGA MAUAJI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 14, 2018

MBUNGE AKAMATWA KWA KUPANGA MAUAJI

  Malunde       Wednesday, March 14, 2018

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Laikipa Mashariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 Machi,2018 kwa tuhuma za kupanga mauaji.

Kwa mujibu wa Polisi wa Laikipa Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia chama cha ODM, atafikishwa mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa zao.

Lampurkel alikamatwa baada ya kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.

Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za kupanga njama hizo za mauaji.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post