VIGOGO WA CHADEMA WAWEKWA MAHABUSU..YUMO MBOWE,MSIGWA,MASHINJI,MNYIKA,MWALIMU, MATIKO

Wakili wa viongozi wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa naye ameungwanishwa na viongozi waliowekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  leo mchana Machi 27, 2018,Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Frederick Kihwelo ameeleza kuwa viongozi hao wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao baadhi hushindwa kutokea.

 Kihwelo amesema Mchungaji Msigwa aliitwa na alipofika polisi naye aliunganishwa mahabusu na wenzake ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na wa Bawacha, Halima Mdee bado hawajafika kituoni hapo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 27, 2018, ambao wote wamewekwa mahabusu.

Viongozi wengine waliofika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na wa Bawacha, Halima Mdee bado hawajafika kituoni hapo.

Viongozi hao waliripoti polisi Machi 22, 2018 na kutakiwa kuripoti leo. Siku hiyo Mdee na Matiko hawakuwepo huku Mnyika na Heche wakihojiwa kwa zaidi ya saa mbili kutokana na kutoripoti siku za nyuma.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.


CHANZO- MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527