TATU MZUKA YAKABIDHI KALENDA 500 KWA JESHI LA POLISI,IGP SIRRO ATOA NENO


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikabidhiwa moja ya Kalenda kati ya 500 zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka,kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano kampuni hiyo Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni mmoja wa wawakilishi Simon Simalenga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya faluna ya Tatu Mzuka kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano Tatu Mzuka, Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni mmoja wa wawakilishi Simon Simalenga.
***


Kampuni ya Bahati Nasibu Tatu Mzuka imekabidhi kalenda 500 kwa Jeshi la Polisi  nchini,kama mwanzo wa uhusiano mwema utakaozaa matunda kati ya Tatu  Mzuka na Jeshi la Polisi. 

Akizungumza na waandishi habari wakati makabidhiano ya kalenda kwa Jeshi la Polisi  mapema jana , Msemaji wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga amesema wameamua  kutengeneza kalenda 500 za Jeshi la Polisi kama sehemu ya kujenga 
uhusiano bora, lakini pia kuendeleza kauli mbiu ya Tatu Mzuka ya  ukishinda Tanzania inashinda pia. 

Maganga amesema wao ni raia wema wa Tanzania hivyo ni nafasi ya pekee kuwa mbele kutokana na kazi ambayo inafanya jeshi la Polisi katika kulinda  watu na mali zao chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro,na  kwamba Kauli mbiu ya Tatu Mzuka “Ukishinda Tanzania inashinda”, 

“Mchezo wa bahati nasibu wameweza kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Temeke  katika kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kuwasaidia wananchi wa Mbande baada ya mapolisi kuuliwa kwa kutokuwa na kituo maeneo ya karibu. " Tumefanya kitu hiki kwa niaba ya washindi wa mchezo wetu wa bahati  nasibu,ambao mpaka sasa wamefikia idadi ya milioni 6 ambao wote  wamehakikishiwa usalama wao na jeshi la polisi.

Mkuu wa jeshi la Polisi (IGP ) Simon Sirro ameeleza kuukubali mchezo wa kubahatisha nchini wa  Tatu Mzuka unaoshika kasi kwa kubadilisha maisha ya Watanzania wengi. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akipokea kalenda za jeshi hilo 
zilizokabidhiwa na viongozi wa Tatu Mzuka kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi, Posta jijini Dar es Salaam juzi."Mmefanya jambo  jema lakini pia mmeonyesha mfano kwa wengine, binafsi nimeguswa na  mwamko wenu, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi," alisema IGP  Sirro. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527