SIMBA WAMTANGAZA WAZIRI TIZEBA

Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara imemtangaza Waziri wa Kilimo Charlse Tizeba kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry Jumatano Machi 7,2018

Taarifa ya Manara imeeleza kuwa Waziri Tizeba ndiye ataongoza maelfu ya mashabiki wa soka nchini watakaojitokeza kwenye uwanja wa taifa kushuhudia mtanange huo.

''Waziri wa kilimo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Charles Tizeba anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanasimba na watanzania kuishangilia Simba kwenye mchezo huo utakaoanza saa kumi na mbili jioni'', imeeleza taarifa hiyo.

Mchezo huo wa hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Afrika kusini. Simba imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa timu ya Gendarmerie Tnale ya Djobouti kwa jumla ya mabao 5-0.

Wakati Simba ikisubiri mchezo wake wa Jumatano wapinzani wao Yanga watakuwa dimbani kesho jioni kuumana na wageni wao Township Rollers ya Botswana kwenye uwanja wa taifa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.