MSAFARA WA POLEPOLE WAPATA AJALI KIGOMA


Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la Kijiji cha Nyamidato, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Vx yenye namba za usajili T150 CWE iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Kibuta wakati wakielekea katika ziara ya kiongozi huyo wilayani Kakonko, mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Kwa mujibu wa Kamanda Otieno, waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.


Polepole amewasili mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527