Wednesday, March 7, 2018

Sheria Mpya : UMRI WA KUANZA KUFANYA MAPENZI ITAKUWA MIAKA 15

  Malunde       Wednesday, March 7, 2018

Ufaransa inatarajia kuweka sheria maalum ya umri wa kuanza kufanya mapenzi kuwa ni miaka 15. Hivyo kufuatia mapendekezo hayo mtu yeyote atakayebainika kufanya mapenzi chini ya umri huo atakuwa amebaka.


Maamuzi haya yamekuja nchini humo mara baada ya madaktari na wanasheria kutoa ushauri wao kuhusiana na umri mtu anaostahili kuanza kufanya mapenzi.

Mabadiliko haya yamekuja kufuatia kesi mbili za hivi karibuni nchini Ufaransa zilizohusisha wanaume waliofanya mapenzi na wasichana waliokuwa na umri wa miaka 11.

Katika sheria ya sasa, kama mtu amekutwa na kosa la kufanya mapenzi na mtu chini ya miaka 15 iwe kwa hiari ama makubaliano, mshtakiwa atahukumiwa kwa kosa la kujamiana na mtoto lakini sio kosa la ubakaji.

Kosa hilo litamlazimu mshtakiwa kutoa kiasi cha dola 87,000 kama sehemu ya adhabu na kwenda jela miaka mitano.

Hukumu ni sawa kwa wanaofanya unyanyasaji kwa watu wazima na watoto lakini kosa la ubakaji huwa lina adhabu kubwa zaidi.Haki miliki ya pichaAFPImage caption

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anaunga mkono mpango huo wa kuweka kiwango cha umri wa kuanza kufanya mapenzi.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 alikutwa hana hatia baada ya ushahidi kueleza kuwa aliyefanyiwa vitendo hivyo hakuwa amelazimishwa wala kupewa vitisho vyovyote.

Hata hivyo wakati msimamo huo ukitolewa huko nchini Ufaransa hali ni tofauti katika maeneo mengine barani Ulaya. Sheria ya kujihusha na mapenzi inaruhusu katika umri tofauti;
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post