MBUNGE LUCY MAYENGA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA UKUNE NA SHULE YA SEKONDARI DAKAMA - KAHAMA


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) ametembelea kituo cha afya Ukune na shule ya sekondari Dakama wilayani Kahama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akiwa katika kituo cha afya Ukune Mheshimiwa Mayenga aliyekuwa ameambatana na viongozi wa UWT amekagua hali ya ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya akina mama na watoto na kusaidia nguvu za wananchi kwa kuahidi kutoa mchango wa mabati 100 pindi jengo hilo litakapoanza kupauliwa mwezi ujao.

Aidha Mayenga aliwaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kuchangia nguvu zao katika shughuli za maendeleo.

Akiongea na wanafunzi wa kike 267 katika shule ya sekondari Dakama ,Mayenga aliahidi kufanyia kazi ombi lao la uhitaji wa vitanda katika bweni kwani wana upungufu wa vitanda.

Aliwaasa wanafunzi hao kuepuka vishawishi kama vile kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi hali ambayo inaweza kusababisha wapate mimba na kushindwa ili kutimiza malengo yao.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akiwa katika kituo cha afya Ukune wilayani Kahama.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akisalimiana na akina mama katika kituo cha afya Ukune na kuwapatia zawadi ya sabuni
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akiwa katika kituo cha afya Ukune
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Lucy Mayenga (CCM) akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wilayani Kahama
Mwanafunzi akikumbatiana na mheshimiwa Lucy Mayenga

Theme images by rion819. Powered by Blogger.