RAIS MAGUFULI KESHO KUFUNGUA BARABARA YA ISAKA - LUSAUNGA NA KIWANDA CHA KAHAMA OIL MILL


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Jumamosi Machi 10,2018 atafanya ziara ya siku moja mkoani Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack amesema rais Magufuli atafanya ziara yake wilayani Kahama.

Amesema akiwa wilayani Kahama,kesho mchana Rais Magufuli atazindua barabara ya kiwango cha lami ya kutoka Isaka kwenda Lusaunga Ushirombo na kufungua kiwanda cha Kahama Oil Mill.

Amesema mheshimiwa rais pia atafanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi wilayani Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Theme images by rion819. Powered by Blogger.