RAIS MAGUFULI AMTUMBUA BLANDINA NYONI SHIRIKA LA NYUMBA - NHC


Rais John Magufuli leo Machi 21,2018 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni.

Taarifa iliyotolewa leo, Machi 21, na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza hilo.

Kwa uamuzi huo wa Rais Magufuli mwenye mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa bodi ya NHC atakuwa ameivunja bodi nzima.

Nyoni aliteuliwa kuitumikia nafasi hiyo Februari 25 mwaka 2017 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mamlaka aliyokuwa nayo aliwateua wajumbe 7 wa bodi hiyo.

Uteuzi wa wajumbe hao ulioanza Machi 23, 2017 ulitakiwa kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu


Theme images by rion819. Powered by Blogger.